Ufunuo wa Yohana 21 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ufunuo wa Yohana 21 (Swahili) Revelation 21 (English)

Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. Ufunuo wa Yohana 21:1

I saw a new heaven and a new earth: for the first heaven and the first earth have passed away, and the sea is no more.

Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. Ufunuo wa Yohana 21:2

I saw the holy city, New Jerusalem, coming down out of heaven from God, made ready like a bride adorned for her husband.

Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Ufunuo wa Yohana 21:3

I heard a loud voice out of heaven saying, "Behold, God's dwelling is with people, and he will dwell with them, and they will be his people, and God himself will be with them as their God.

Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. Ufunuo wa Yohana 21:4

He will wipe away from them every tear from their eyes. Death will be no more; neither will there be mourning, nor crying, nor pain, any more. The first things have passed away."

Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli. Ufunuo wa Yohana 21:5

He who sits on the throne said, "Behold, I am making all things new." He said, "Write, for these words of God are faithful and true."

Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure. Ufunuo wa Yohana 21:6

He said to me, "It is done! I am the Alpha and the Omega, the Beginning and the End. I will give freely to him who is thirsty from the spring of the water of life.

Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. Ufunuo wa Yohana 21:7

He who overcomes, I will give him these things. I will be his God, and he will be my son.

Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili. Ufunuo wa Yohana 21:8

But for the cowardly, unbelieving, sinners, abominable, murderers, sexually immoral, sorcerers,{The word for "sorcerers" here also includes users of potions and drugs.} idolaters, and all liars, their part is in the lake that burns with fire and sulfur, which is the second death."

Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo. Ufunuo wa Yohana 21:9

One of the seven angels who had the seven bowls, who were loaded with the seven last plagues came, and he spoke with me, saying, "Come here. I will show you the wife, the Lamb's bride."

Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu; Ufunuo wa Yohana 21:10

He carried me away in the Spirit to a great and high mountain, and showed me the holy city, Jerusalem, coming down out of heaven from God,

wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri; Ufunuo wa Yohana 21:11

having the glory of God. Her light was like a most precious stone, as if it was a jasper stone, clear as crystal;

ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli. Ufunuo wa Yohana 21:12

having a great and high wall; having twelve gates, and at the gates twelve angels; and names written on them, which are the names of the twelve tribes of the children of Israel.

Upande wa mashariki milango mitatu; na upande wa kaskazini milango mitatu; na upande wa kusini milango mitatu; na upande wa magharibi milango mitatu. Ufunuo wa Yohana 21:13

On the east were three gates; and on the north three gates; and on the south three gates; and on the west three gates.

Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo. Ufunuo wa Yohana 21:14

The wall of the city had twelve foundations, and on them twelve names of the twelve Apostles of the Lamb.

Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake. Ufunuo wa Yohana 21:15

He who spoke with me had for a measure, a golden reed, to measure the city, its gates, and its walls.

Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa. Ufunuo wa Yohana 21:16

The city lies foursquare, and its length is as great as its breadth. He measured the city with the reed, Twelve thousand twelve stadia{12,012 stadia = or 2,221 kilometers or 1,380 miles. TR reads 12,000 stadia instead of 12,012 stadia.}. Its length, breadth, and height are equal.

Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika. Ufunuo wa Yohana 21:17

Its wall is one hundred forty-four cubits,{144 cubits is about 65.8 meters or 216 feet} by the measure of a man, that is, of an angel.

Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi. Ufunuo wa Yohana 21:18

The construction of its wall was jasper. The city was pure gold, like pure glass.

Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi; Ufunuo wa Yohana 21:19

The foundations of the city's wall were adorned with all kinds of precious stones. The first foundation was jasper; the second, sapphire{or, lapis lazuli}; the third, chalcedony; the fourth, emerald;

wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto. Ufunuo wa Yohana 21:20

the fifth, sardonyx; the sixth, sardius; the seventh, chrysolite; the eighth, beryl; the ninth, topaz; the tenth, chrysoprasus; the eleventh, jacinth; and the twelfth, amethyst.

Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu. Ufunuo wa Yohana 21:21

The twelve gates were twelve pearls. Each one of the gates was made of one pearl. The street of the city was pure gold, like transparent glass.

Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake. Ufunuo wa Yohana 21:22

I saw no temple in it, for the Lord God, the Almighty, and the Lamb, are its temple.

Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo. Ufunuo wa Yohana 21:23

The city has no need for the sun, neither of the moon, to shine, for the very glory of God illuminated it, and its lamp is the Lamb.

Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake. Ufunuo wa Yohana 21:24

The nations will walk in its light. The kings of the earth bring the glory and honor of the nations into it.

Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku. Ufunuo wa Yohana 21:25

Its gates will in no way be shut by day (for there will be no night there),

Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake. Ufunuo wa Yohana 21:26

and they shall bring the glory and the honor of the nations into it so that they may enter.

Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo. Ufunuo wa Yohana 21:27

There will in no way enter into it anything profane, or one who causes an abomination or a lie, but only those who are written in the Lamb's book of life.